SHOSTI
DEOGRATIUS GIFT KIPAPA
Mvua ilinyesha siku hiyo, kama kawaida ya jiji la dar es salaam bara bara zilikuwa hazipitiki kabisa,
Na kwa wafanya biashara waliokuwa wanafanyia bishara zao kando kando ya bara bara wao adha hiyo ndio iliwapata mara mbili, bidhaaa ziliharibiwa na matope, miundo mbinu ilikuwa migumu kwa wateja wao kusogea jirani na bidhaa zao yani ilikuwa kero tupu.
“acha kunichekesha shosti kwa hiyo ukaamua kumu unfriend kabisa?”
“kwani mi nafuga ujinga? Tena hata hazikupita dakika mbili shenzi, ile ananitafuta tu inbox anapewa notification kwamba anatakiwa kuniomba urafiki ili kuchati na mimi, akaanza kulia lia kwenye simu eti ‘oooh, switiii jamani, ndio umenikasikirikia kiasi hicho hadi unanitoa urafiki?’ nikamwambia ndio utanyooka mbwa wewe, unafikiri mimi nashabikia huo upuuzi wako?”
Walipiga stori hizo wasichana wa shule ya sekondari, wakiingiia kwenye bara bara wakitokea kwenye kichochoro na sare zao za shule , kulikuwa na bango la shule yao upande ule bango hilo lilikuwa limebeba ujumbe ulioandikwa, ‘elimu ni taa ya maisha, soma ili usitembee gizani.’
Sare zao za shule ndio ilikuwa komeshea, vilikuwa ni visketi vifupi kama vimini kabisa yani , vilikuwa vinaishia usawa wa magoti alafu vimebanwa hivi kuendana na shepu zao kabisa, vishati navyo vilikuwa vidogo dogo zile wanaita small size, basi watoto wa kike na vile walivyokuwa wamemetisha kwa soksi nyeupe viatu vinangara kwa kiwi ya kangaroo, na miili yao vile ilivyokuwa midogo dogo, si unajua tena uzuri huwa unawapataa wasichana wote wakiwa katika umri wa miaka kumi na tano na kumi na sita, basi kwa hawa watoto wa shule waliokuwa na rangi za asili bado, mmoja weusi wake ulikuwa unang’ara hivi kama chokleti na huyo mwenzake alikuwa na maji ya kunde yaliyoiva , basi wakitembea hivi hiyo miguu yao walivyokuwa wanaitoa kwa kumetisha mwendo wa maringo kama kinyonga utadhani wale warimbwende wa kwenye mashindano ya umisi wakiwa kwenye jukwaa la miondoko.
Mmoja ndio alikuwa na guuu guuu , akipita mbele yako mtoto wa kiume huwezi hata kungoja ageuke, kudata lazima udate sio siri warembo hawa walikuwa wanajua kujichetua.
“alituma kadi tano kwa siku!?”
“tena zote nikazichana mbele yake, akaanza kujiliza pale na vingereza vyake sijui ‘ooohh, switii I was give you all my heart, you’re my one and only, nikamwambia kwenda huko na huo uchizi wako, kapeleke huko ka maboya wenzako!!”
Alizidi kusimulia mrembo huyo, mwenzake alikuwa hana mbavu kwa kicheko, waliendelea kutembea kando kando ya bara bara hiyo wakikwepa hivi maeneo yenye matope mengi.
“hey totoz mamboz!!”
Ilisikika sauti hiyo ya mwanaume aliyekuwa ndani ya gari moja aina ya Noah ya rangi nyeusi, mpya new! Vioo vyake vilikuwa na tintedi, mwanaume huyo alifungua hivi kioo cha siti ya nyuma aliyokuwa amekaa, mbele kulikuwa na dereva aliyekuwa anaendesha gari hilo taratibu, nae pia macho yake yakiwa yamekazana kuwacheki watoto hao kwenye saiti mila.
“poa!! poa!”
alijibu mmoja kati ya warembo hao, yule aliyekuwa anapigisha stori mwenzake.
“ poa poa sio! Kwanini msiiingie ndani ya gari niwape lifti eeeh, mtachafua hizo unifomu na matope haya au mnasemaje watoto wazuri!?”
Aliongea mwanaume huyo huku akiendelea kuwathaminisha vizuri uzuri wao akianzia chini na kunyanyuka hivi, yani mpaka akawa anainamisha hivi miwani yake, ili apate kujionea uzuri watoto hao kwa macho yake yote mawili mubashara.
0 comments:
Post a Comment