Search This Blog

USIMWAMBIE DADA

 


USIMWAMBIE DADA 

By Deogratius Giftkipapa

MWANZO WA STORI:
Ilikuwa nyumba nzuri ajabu, ngazi zake zilikuwa nene nene hivi, kibaraza sasa juu na chini vyote vilikuwa vimejengwa kwa zege nzito, alafu nyumba nzima ilikuwa imepakwa rangi nyeupe pee kama white house ‘ikulu’.
Pembeni kulikuwa na taa zilizobuniwa kwa mtindo mtindo, umbo lake lilikuwa ni pembe tatu hivi lakini duara kwa ndani, madirisha yalikuwa mapana yote yalikuwa ya vioo, yakiwa wameshikizwa kwa vyuma vyenye madini ya alminium. Lakini ndani kulikuwa na pazia la rangi nyeupe, hadi vyungu vya maua vilivyopangwa kando kando ya kibaraza kilichozunguka nyumba hiyo navyo pia vilipakwa rangi nyeupe.
Vijinjia vilivyokuwa vinapita kukatisha viunga vya bustani vilikuwa vimejengwa kwa vijitofali fulani hivi vyenye nakshi nakshi lakini rangi yake ilikuwa nyeupe, hata vijitofali vilivyopangwa kuzunguka bustani hiyo navyo pia vilipakwa rangi nyeupe karibu kila kitu kilikuwa cheupe hapo hata sijui mmiliki wa nyumba hiyo ana tatizo gani na rangi nyeupe.
Kasoro viti vilivyopangwa pembezoni mwa bwawa la kuogelea pamoja na sanamu ya mwanamke aliyekuwa uchi iliyowekwa pembezoni mwa bwawa hilo ndio pekee havikuwa na rangi nyeupe.
Mito ya viti ilikuwa na rangi nyeusi wakati fremu yake ilikuwa na rangi yake ya mbao sema iringa’arishwa na vanishi na kuifanya ivutie zaidi. Sanamu ilikuwa na rangi ya kahawia, lakini eneo la kucha lilipakwa nyeupe na nywele nyeusi yani kama mtu kweli vile, ukicheki matiti yalikuwa yamesimama hivi na chuchu zake kama kifuu cha nazi.
Mguu mmoja wa sanamu hiyo ulichongwa kwa kusogea mbele kidogo utafikiri mwana dada mlimbwende anataka kuingia ndani ya bwawa la kuogelea.
Rangi ya weupe wa nyumba, mawingu ya angani pamoja na ukijani wa vichaka vilivyopandwa kwenye bustani vyote vilikuwa vinaonekana ndani ya maji yaliyokuwa ndani ya bwawa kama picha.
Upande wa pili wa bwawa hilo kulikuwa na msichana amelala kifudi fudi kwenye benchi, alikuwa na miguu mizuri kinyama, kisigino softi kama vile hajawahi kukanyaga chini katika maisha yake yote. Guu, guu mtoto wa kike, ukisikia mguu wa bia basi ndio huo.
Matako kudadeki walai mrembo alikuwa na matako ya kuvutia kinyama. Tena vile alivyokuwa amevaa kijigauni cha kuogelea, yani chini chupi tu tena kichupi chenyewe kama bikini, sababu kilikuwa na kikamba fulani kilichopita kati kati ya matako yake, pale pale kwenye mstari wa ikweta, alafu vile kigauni hicho kilivyokuwa kimetaiti basi hata kikamba hicho kilikuwa akionekani katikati ya matako hayo kitendo kilicho yafanya matako yake yanoge kisenge.
Maji maji yaliyokuwa yamelirowesha tako hilo yalilifanya limelemete kwa kumurikwa na mwanga wa jua, eneo la mgongo wake nao lilikuwa wazi, kama matakoni napo kuna vikamba kamba fulani vilipita kupanda juu kuyashikilia matiti yake, uso wa mrembo huyo ulionekana kichwani alikuwa amesuka msuko mmoja wa hatari .
yani unaweza kusema njia tatu fulani lakini yeye jinsi alivyokuwa na unywele mtoto wa kike hakusukia rasta bali nywele zake mweyewe, kwa chini zilishuka kama mikia miwili iliyokuwa inafika mpaka mgongoni.
Masikioni kwake alikuwa ametia earphone akisikiliza muziki uliomfanya akitikise kichwa chake hivi kiupande upande.
Mdomo wake mzuri uliokuwa unacheza cheza hivi lipsi na ulimi viligongana. Macho yake alikuwa ameyafumba kwa hisia, kidevu na pua yake navyo viliyumbishwa hivi pamoja na kichwa chake hivi taratibu, wimbo huo ulikuwa umeiteka akili ya mrembo huyo yote.

0 comments:

Post a Comment

Blog