BY GIFT KIPAPA
MWANZO WA STORI:
Yalikuwa majira ya saa tano asubuhi, pirika pirika pirika zilikuwa karibu kila kona ya jiji la dar es salaam, mahoteli yalijaa watu waliokuwa wanapata kifungua kinywa, lakini kaunta zote za bar zilifungwa, ilikuwa sheria ya nchi ‘marufuku kunywa pombe muda wa kazi’ mheshimiwa alisema, na hiyo ndio ilikuwa kanuni ya nchi nzima. Lakini kulikuwa na pub moja ya siri, ilikuwa imejengwa kwa ndani hivi, hakuna muziki wala kelele za aina yoyote, ni kaunta na vinywaji, hata mwanga ulikuwa hafifu, wateja wengi walipokuwa wanakuja kwenye baa hiyo ni wale wasiopenda usumbufu. Na pia waliuza nyama choma na mchemsho lakini hivyo vilikuwa vinaandaliwa kwenye bara yao kubwa iliyokuwa ng’ambo tu ya bara bara ya mtaa huo uliokuwa umejaa pirika za kila aina kama unavyoijua kariakoo, huyu atauza simu, mwingine mikoba ya ngozi, na hata feki wote walikuwa wakizunguka hivi huwezi jua upi mdosho au upi ni orijino, pembeni maduka mengine yalikuwa yamepangana, vifaa vya kielekitroniki na mavazi ndio vilikuwa vimetawala na watu kibao waliingia na kutoka kwenye maduka hayo wakijipatia mahitaji yao.
Kulikuwa na hili gari la kifahari aina ya harrier new model, rangi nyeusi iliyokuwa inang’ara hivi ilisogea taratibu kwenda kupaki kwenye maegesho ya hoteli hiyo kubwa yenye roshani ya ghorofa kama saba hivi, kibao kiliandikwa ‘TOUCH TOUCH MOTEL’ madirisha yake ya vioo yalionyesha ndani wateja waliokuwa eneo la restaurant wakipata chochote kitu.
Gari hilo lilipoegeshwa, milango ilifunguliwa, wasichana wawili wazuri umri wao ulikuwa kama miaka thelathini na tano na saba hivi, mavazi yao yalikuwa ni ya kisista duu, vigauni Fulani hivi vifupi usawa wa mapajani matirio yake ni ya mterezo Fulani vilivyoshikana na maungo yao akitembea hivi matako yalikuwa yanatikisika kinoma.
Walikuwa wanapiga stori wakizungumzia jambo Fulani njia mzima, mmoja aliyekuwa amevalia kigauni chenye rangi nyekundu kama mtoko wa valentine ndio alikuwa muongeaji zaidi na mwenzake alimsikiliza na kucheka vituko alivyokuwa anamuonyesha.
Badala ya kuingia ndani ya hoteli hiyo, walivuka bara bara kuingia ndani ya ile grocery iliyokuwa imejificha kati kati ya maduka .
Waliingia ndani ya grocery hiyo, ilikuwa kimya kuliko hata unavyoweza kudhania, kelele zote na pirika pirika za watu kutoka na kuingia madukani ziliishia nje, humo ndani mlifungwa vifaa vya kuzuia sauti kutoka na kuingia ndani, alafu hali ya hewa ilikuwa ya ubaridi fulani hivi yani huwezi hata kuwaza kama upo ndani ya jiji la dar es salaam si unajua mambo ya kiyoyozi.
“karibuni wateja.”
Mhudumu aliwakaribisha walipokuwa wanapiga hatua kusogea eneo la kaunta, alikuwa ni mwanaume mmoja mwenye muonekano wa kuvutia kinyama, alikuwa na tatuu ya jembe likiwa limeinuliwa hivi kulima kipande cha ardhi kwenye mkono wake wa kushoto na kichwani rasta zile za kisasa zinazosukiwa hivi na urembo rembo Fulani na kupakwa rangi.
0 comments:
Post a Comment