Search This Blog

MSICHANA WA NYUMBA YA PILI

 



MSICHANA WA NYUMBA YA PILI
GIFT KIPAPA
The damn writer!
Bustani nzuri ya maua na miti iliyokuwa yamepandwa kwa mpangilio mzuri mno, nyasi zilikuwa zimekatwa kwa ustadi utazani limetandikwa kapeti.
nyumba nzuri iliyopakwa rangi kwa nakshi, nakshi, nashi, huo ulikuwa muonekano wa nyumba zote zilizokuwa katika mtaa huo tulivu, walikuwa wanaishi washua tupu hakuna cha mlinzi wa geti wala mtunza bustani aliyekuwa anazengea katika mitaa hiyo wote walikuwa wanafanya kazi kwa apointimenti maalumu, akikafanya usafi asubuhi na mapema anasepa zake, chakula kilikuwa kinaagizwa kwa simu katika migahawa yenye apps zinazo chukua oder na kupokea malipo online.
Kutoka upande wa pili wa bara bara mwanamke mmoja alichepuka kwenye kijinjia kilichosakafiwa kukatiza kati kati ya bustani ya moja kati za nyumba hizo za mtaani hapo.
Mkononi alikuwa ameshika keki iliyokuwa imetengenezwa vizuri kwa vanilla na chokoleti na mapocho pocho mengine yenye utamu kunoga.
Alikuwa amevaa gauni la kulalia ambalo linafungwa kamba kiunoni, matiti ya mwanamke huyo yalikuwaayakionekana kiana vile yalivyokuwa yanatikisika akitembea kwa haraka kuukaribia mlango wa nyumba hiyo.
Viatu vyake vilikuwa vinatoa mlio wa konko nko wakati nywele zake zilizokuwa zimechanwa vizuri kwa kulazwa hivi kiupande upande kwenye kichwa chake zikiwa zinacheza cheza na kujisugua sugua kwenye kora ya gauni la mwanamke huyo.
Aliufikia mlango wa nyumba hiyo uliokuwa na boxi la kupokelea barua pamoja na kengele ya umeme kwaa ajili ya kubishia hodi lakini mwanamke huyo aliamua kugonga mlango huo kwa mkono wake.
Aligonga kama mara tatu hivi mfululizo na kisha kusubiri, akiwa ameishikilia keki yake kwa mkono mmoja na kujichezesha chezesha hivi mwili wake.
Zilipita kama sekunde mbili tatu hivi kisha mlango huo ulifunguliwa, mwanaume alitokeza.
“Ha-ba, haba-ri, ha-ba-ri ya woooo?”
Aliongea mwanaume huyo kwa kigugumiza na mshangao mkubwa, huku akitoka nje na kuufunga mlango kwa mkono wake wa mwisho kutoka, uzuri wa mwanamke huyo ndio uliomfanya ajing’ate ng’ate kutoa salamu yake, matiti ya mwanamke huyo vile yalivyokuwa yanaonekana na uso wake ilikuwa balaa.
Ni kweli alitoka nje kwa kutarajia mgeni, lakini sio mgeni wa kike mwenye uzuri wa kiasi hicho.
“habari yako .”
Aliongea mrembo huyo kwa sauti yake laini na tabasamu lilioufanya uso wake unoge ile kinoma.
“Habari yangu nzuri tu.”
Aliitikia mwanaume huyo huku akiendelea kuukodolea macho uzuri wa mwanamke huyo.
“safi, jina langu ni dina ni jirani wenu kutoka nyumba ya pili hapo, nimekuja kuwa karibisha mtaani kwetu, nimewatengenezea keki .”
Aliongea dina huku wakijichezesha chezesha hivi mwili wake, kuonyesha sehemu za mwili wake zilizokuwa na mvuto , paja lake alikuwa kama vile analitoa nje ya gauni hiyo, nywele zake kichwani zilicheza cheza hivi taratibu huku mkono wake mmoja akiwa kama anajifunua gauni lake eneo la matiti ili yatoke hivi kwa nje na chuchu za matiti hayo zilionekana, ulimi wake ulikuwa ukicheza cheza kuziramba lipsi za midomo yake aliyokuwa anaipindisha pindisha kwa staili fulani utafikiri anapata radha fulani ya kulalama hivi kama anakunwa.
Unaweza kudhani yeye ndio hiyo keki anayoizungumzia.

0 comments:

Post a Comment

Blog