BY GIFT KIPAPA
“Toka nyumbani kwetu kumamako, toka lazima uhame leo mbwiga wewe, unajifanya mpangaji kumbe unamlia mingo maza bafuni, toka nimesema!!”
“hebu niache huko yasin, achia taulo langu dogo, acha huko!!!”
“yasin, yasin hebu mwache, yasin ukimvua hilo taulo na mimi khanga yangu navua, eeeh si unataka laana, watu wote uliowajaza hapa wanauona uchi wangu leo, mvue, mvue hilo taulo uone , kama sijakutia laana mjinga wewe.”
“anavua anavua mama yasini nae anavua khanga ooyoooo , tunajionea video ya bure leo, ooyoo.”
“cheki paja cheki paja lile lilivyo jeupe kumamakooooo walai Ntuli ana haki ya kukamatia jimama weee!! Weeeeeee!!!”
Kilikuwa kisanga cha kwanza kufungulia siku mtaani, watu walijazana kwenye uwanja wa kina yasin utadhani kulikuwa na shughuli, hadi wale wanawake wanaouza vitafunio mtaa wa pili walikuwa hapo vitu vyao sijui hata walimuachia nani.
“acha, hembu acheni ujinga huko , mama yasin hebu jifunike khanga hiyo, na wewe yasin hebu achia taulo la ntuli acheni wenda wazimu wenu , mnataka majirani watuanagalieje sisi , hebu acheni huo utahila wenu hebo!!!?
Mwanaume mmoja alifoka mara baada ya kufika hapo.
“bora mjomba umekuja, huyu bwege alikuwa anamkaza maza bafuni .”
Yasin aliropoka kwa hasira mkono wake bado ulikuwa umeshikilia taulo la ntuli , akilivuta vuta hivi.
“nimesema achia taulo lake, usikii, sijali ni nini alichofanya, Ni mesema acha, yasini nitakutia vibao sasa hivi acha usikii!”
Alizidi kufoka mjomba.
”kweli kaka licharaze viboko kabisa manaake toto bishi kama nini, lione kwanza bichwa lake maji kama baba yake.”
Mama yasin aliropoka, wakati kaka mjomba akihangaika kumvuta hivi yasin, alimpiga kofi moja la nguvu shingoni
‘pwaaaa’
lilikuwa kofi kofi haswa, yasin alijisikia kizungu zungu Fulani hivi na kuyumba yumba kidog , Lakini taulo bado hakuliachia, kofi lingine lilifuata
‘pwaaaa’
na lingine
‘pwaaaaa’
hili sasa ndio lilikuwa kofi takatifu , yasin bila kupenda aliachia taulo la ntuli, huku machozi mfululizo yakimbubujika.
“sawa tu mjomba mi nionee tu, umeona sababu baba yangu hayupo mjomba sawa.”
Alilia yasini akisikilizia maumivu ya makofi aliyotwangwa.
“baba yako kitu gani? Kwani uliambiwa yeye ndio alitoa mali hapa, kama sio kuzuga zuga na vimia mbili mia mbili vya bangi zake na mwisho wa siku kaishia segerea.”
mama yasin alimpasha mwanae akiyatikisa hivi matako yake na kukitikisa kidole chake cha kati kama vile yupo kutoa michambo ya kishambenga kwenye msuto na wanawake wenzake.
“mpe mpe huyo habari yake mama yasin.”
Wanwake waliokuwa pembeni walishangilia kujaza misifa kwenye kichwa cha mama yasin.
“hebu tulia huko na wewe, usitake kuleta leta kimdomo chako, ingia ndani , mmamam mtu mzima kazi kuhangaika na wavulana wadogo , huyu si sawa na mwanao kabisa.”
Alifoka mjomba yake yasin.
“eeehh , Na we kaka hebu nipishege mie huko , kwani we hujui kwamba tete teke tamu.”
mama yasin alimtupia kaka yake maneno hayo makavu kwa staili yake ile ie ya kimichambo.
“weeeeee, wape wape vidonge mama yasin, halo ya teke tekeeeeee, aaahhh, aaahhh.”
Wanawake walipiga yowe, wakinyanyua mikono yao juu kishambenga na kutikisa matako yao kama vile wapo kucheza muziki wa taarabu kwenye kigodoro.
Mjomba hasira zilimpanda wala hata hakuwa na ujasiri wa kuweza kuvumilia upuuzi huo, alimuachia yasin na kutoka nduki ili amkamate mama yasin pale alipokuwa amesimama, mama yasin alipomuona tu nae alikurupuka kukimbia.
“mama, mama uwwiii, uwiii, nisamehe kaka nisa…”
Alipiga kelele hizo mama yasin huku akikimbia kuelekea kichochoro kinacho elekea barabarani kwenye nyumba yao ya pili wanakokaa wapangaji tupu, khanga yake ilidondoka chini, hapo sasa ndio mambo yalikuwa mambo, mama yasin alikuwa uchi wa mnyama hakuvaa cha chupi wala nini , basi vile tako lake lilivyokuwa linatikisika, kwa wambea wa mtaani ilikuwa balaa.
Watu walishanglia kinoma, mjomba nae bila aibu aliendelea kumkimbiza dada yake akiwa uchi wa mnyama, walivuka barabara ya mtaa, nyuma yao watu kibao walikuwa wakikimbilia kushuhudia tukio, huku wakipiga makelele wakishangilia kuuona uchi wa mama yasin hadharani.
0 comments:
Post a Comment